KUTEMBELEA - MIRERANI

Meja Jenerali Michael Isamuhyo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa maelezo wakati alipotembelea eneo la vitalu A mpaka D kwenye machimbo ya tanzanite Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara jana. Jeshi hilo limeagizwa na Rais John Magufuli juzi kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kudhibiti wizi wa madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee. (Picha na Ikulu).

Add a comment

SHADA LA MAUA

Spika wa Bunge, Job Ndugai akiweka shada la maua katika maziko ya watu watano wa familia ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa) wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).

Add a comment

KUZUNGUMZA

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker ambaye alifika Ofisini kwa Makamu wa Rais jana, Ikulu Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Add a comment

WATUMISHI - GAIRO

Watumishi wa halmashauri ya Gairo na Kilosa, mkoani Morogoro wakiwa nje ya eneo la mkutano baada ya kukutana na viongozi wakuu wa serikali hivi karibuni mjini Gairo, mkoani humo. (Picha na John Nditi).

Add a comment

KUKATA UTEPE

Rais John Magufuli na viongozi wengine akikata utepe kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara jana. (Picha na Ikulu).

Add a comment

KUELEZA

Kaimu Mhariri wa gazeti la HabariLeo, Nicodemus Ikonko (kushoto) akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia viongozi wakuu Zanzibar kuhusu hatua za uandaaji wa gazeti hilo wakati wajumbe hao pamoja na watendaji wa Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar walipotembelea Makao Makuu ya ofisi za kampuni hiyo yaliyopo Barabara ya Mandela, Dar es Salaam., Dar es Salaam jana. (Picha na Fadhili Akida).

Add a comment