HabariLeo Mobile Edition

Back Home

KCC yachomoza Kombe la Mapinduzi

TIMU ya soka ya KCC ya Uganda jana ilianza vema michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuwafunga wenyeji KMKM kwa mabao 3-2 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, KCC walikuwa mbele ya mabao 2-1.

Mabao ya KCC yalifungwa na Herman Maswa, Tony Odur na William Waogo. Mabao ya KMKM yalifungwa na Khamisi Ally na Maulid Ibrahim Kapenta.

Nao Mbeya City ilitoka sare ya bao 1-1 na Clove Stars.